MBEYA-Katika harakati za kupunguza uhitaji wa dawa za kulevya nchini, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa Kulevya (DCEA) imetoa elimu kwa viongozi wa serikali za mitaa 17.
Ni iliyotajwa kuwa na changamoto kubwa ya matumizi na biashara ya dawa za kulevya pamoja na viongozi wa asasi zinazotoa huduma kwa waraibu jijini Mbeya.Mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uelewa wa kina kuhusu tatizo la dawa za Kulevya, madhara ya dawa hizo na nafasi yao katika kutokomeza dawa za Kulevya kwenye maeneo yao.
Pamoja na elimu hiyo, viongozi hao walihimizwa kushirikiana kwa karibu na DCEA katika kutoa taarifa za matumizi na biashara ya dawa za kulevya kupitia namba 119 bila malipo.
Vilevile,kushiriki kikamilifu katika operesheni za kudhibiti dawa hizo na kutoa ushahidi mahakamani pale inapohitajika.
Tags
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Kataa Dawa za Kulevya na Timiza Ndoto Zako
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)





