SINGIDA-Wizara ya Fedha imeng'ara kwenye Sherehe ya Wafanyakazi (Mei Mosi) Kitaifa, baada ya kuwa mshindi wa kwanza wa mchezo wa mpira wa miguu katika mashindano yaliyoshirikisha Wizara na Taasisi za Serikali.

Akizungumza wakati wa maandamano ya wafanyakazi wa Wizara ya Fedha walioshiriki katika sherehe hizo, Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) Wizara ya Fedha, Bw. Shumbi Mkumbo, alisema kuwa Wizara ya Fedha imenyakua tuzo mbili ikiwemo hiyo ya mshindi wa mpira wa miguu na tuzo ya uendeshaji Baskeli, jambo lililo chochea hamasa kwa watumishi wa Wizara kushiriki zaidi katika michezo.
Alisema kuwa Wizara itaendelea kuhamasisha michezo kwa kuwa inaimarisha afya kwa watumishi na pia inahimiza umoja na mshikamano.