DAR-Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) kimemchagua,Yustas Rwamugira kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba,mwaka huu.
Hatua hiyo imefikiwa katika Uchaguzi Mkuu wa chama hicho uliofanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi wa chama hicho Mei 26,2025 Mwenyekiti wa uchaguzi huo Coaster Jimmy, amesema jumla ya wapiga kura walikuwa 103.
Kati ya hizo Yustas Rwamugira ambaye ni Katibu Mkuu wa TLP amepata kura 51 huku washindani wenzake Neema Nyerere akipata kura sita,Wilson Ellas kura 46.
Yustas Rwamugira amewashukuru wanachama kwa kuonesha imani kubwa kwake huku akiahidi kuwa yeye na mgombea mweza wake, Amana Selemani Mzee watakiwakilisha vema chama hicho.
Msajili Msaidizi wa vyama vya Siasa Tanzania, Sisty Nyahoza amewapongeza Tanzania Labour Party TLP, kwa kufanya uchaguzi kwa amani wa chama hicho huku akiwatakia kila la heri.
Tags
Habari
Siasa za Tanzania
Tanzania Labour Party (TLP)
Uchaguzi Mkuu 2025
Vyama vya Siasa
Yustas Rwamugira
