MARA-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar itaendelea kuimarisha Ushirikiano wa kiuchumi na Diplomasia na Msumbiji kwa manufaa ya nchi hizo mbili.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipokuwa na Mazungumzo na Rais wa Msumbiji Daniel Francisco Chapo ambaye yupo nchini kwa ziara maalum yaliofanyika Ikulu, Zanzibar tarehe 9 Mei 2025.Aidha Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa uamuzi wa kufanya ziara ya Kwanza Tanzania ikiwemo Zanzibar baada ya kuchaguliwa kunaonesha kuthamini Ushirikiano huo ulioasisiwa na Viongozi Waasisi wa Mataifa hayo.
Rais Chapo ameeleza kuwa ziara hiyo itafungua milango na fursa za kiuchumi baina ya nchi hizo pamoja na uhusiamo wa kidiplomasia wa muda mrefu.








