ZANZIBAR-Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) limevitaka vilabu vya mpira wa miguu Zanzibar kuacha mara moja tabia ya kwenda viwanjani na vikundi maalum vya kucheza vya wanawake visivyo na maadili, ambao huvaa mavazi yanayoonesha maumbile yao.
ZFF imesema itazichukulia hatua kali na stahiki timu zote zinazopeleka vikundi hivyo uwanjani kwani ilishakatazwa na Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar (BTMZ).

