IRINGA-Zimebaki siku nne kuanza kwa Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Tanzania kwa Shule za Msingi na Sekondari nchini (UMITASHUMTA na UMISSETA 2025) yanayotarajiwa kufanyika kitaifa Mkoani Iringa.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa, anatatajiwa kufungua rasmi Mashindano hayo tarehe 9 Mei 2025 ambapo zaidi ya wanamichezo 7,000 kutoka mikoa mbalimbali nchini watahusika kwenye Michezo ya mwaka huu.
Kauli mbiu ya Mashindano ya mwaka huu ni "Viongozi bora ni msingi wa maendeleo na Taaluma, Sanaa na Michezo, Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na Utulivu."
UMITASHUMTA na UMISSETA 2025 inaandaliwa na kusimamiwa na OR-TAMISEMI ikishirikiana na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, na Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo.