MAPUTO-Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji ambaye pia anawakilisha Madagascar na Ufalme wa Eswatini, Mheshimiwa CP. Hamad Khamis Hamad amekutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Malek Djaoud, Balozi wa Jamhuri ya Algeria nchini Msumbiji kwenye ofisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo jijini Maputo.
Katika mazungumzo yao, pamoja na masuala mengine, Mabalozi hao waligusia umuhimu wa kuendeleza mahusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Msumbiji.







