MAPUTO-Juni 19,2025 Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji anayewakilisha mataifa ya Madagascar na Ufalme wa Eswatini,Mheshimiwa CP Hamad Khamis Hamad amekutana na Wawakilishi wa Diaspora waliopo Maputo kwenye Viwanja vya Ubalozi jijini Maputo.
Katika mkutano huo, mbali ya kupokea changamoto zinazowakabili Diaspora hao, aliwasisitiza kuwa raia na mabalozi wema kwa muda wote watakapokuwa Msumbiji.Aidha, aliwahakikishia kwamba Ubalozi utatoa kila aina ya msaada na ushirikiano katika kutatua changamoto zao.



