MAPUTO-Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji ambaye pia anawakilisha Madagascar na Ufalme wa Eswatini,Mheshimiwa CP Hamad Khamis Hamad amekutana na Mhe. Philip Githiora, Balozi wa Jamhuri ya Kenya nchini Msumbiji na kuzungumza masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya. Mazungumzo hayo yamefanyika Juni 11,2025 jijini humo.

