MBEYA-Katika kuadhimisha miaka 59 tangu kuanzishwa kwa Benki Kuu ya Tanzania, Tawi la Benki Kuu Mbeya limetoa msaada wa vifaa na mahitaji mbalimbali kwa taasisi za kijamii katika mkoa huo.
Msaada huo umejumuisha viti 25 na meza 12 kwa Shule ya Msingi Itiji, mashuka 200, mashine moja ya kupima shinikizo la damu (BP machine), pamoja na viti vitatu vya magurudumu kwa Hospitali Teule Mbalizi.
Aidha, msaada wa chakula umetolewa kwa Kituo cha Watoto Yatima cha HOPE, ikiwa ni sehemu ya mchango wa benki katika kuunga mkono jamii inayoizunguka.