DAR-Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imetangaza maofisa wa mchezo wa Dabi ya Kariakoo kwenye Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kati ya wenyeji Young Africans SC dhidi ya Simba SC.
Taarifa ya bodi imebainisha kuwa, mchezo huo namba 184 utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Misri.
Pia, taarifa hiyo imebainisha kuwa,Mwamuzi wa kati atakuwa Amin Mohamed Amin Omar kutoka Misri akisaidiwa na Mahmoud Ahmed Abo El Regal kama Mwamuzi msaidizi namba moja na Samir Gamal Saad Mohamed ambaye atakuwa msaidizi namba mbili.
Aidha,Kamishna wa mchezo huo utakaopigwa Juni 25, 2025 saa 11:00 jioni katika dimba la Benjamin Mkapa anatarajiwa kuwa Salim Omary Singano.