DAR- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuhamisha Kenan Laban Kihongosi kutoka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha akichukua nafasi ya Paul Christian Makonda.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Taarifa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais (Ikulu) Juni 23,2025 haikutoa taarifa zaidi kuhusu Paul Makonda.