Dkt.Natu El-maamry Mwamba afanya mazungumzo na ujumbe kutoka Benki ya Dunia

DODOMA-Katibu Mkuu Wizara ya Fedha,Dkt. Natu El-maamry Mwamba amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Benki ya Dunia kuhusu ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Benki hiyo, kikao ambacho kilifanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square jijini Dodoma.
Katika kikao hicho wamejadiliana kuhusu kuendeleza mageuzi ya kimfumo yanayolenga uthabiti wa kiuchumi, uboreshaji wa fedha za umma, uhimilivu wa deni la serikali, kukuza sekta binafsi katika ujumuishaji wa kijamii katika masuala ya kiuchumi na uangalizi wa mabadiliko ya tabianchi.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Kamishna wa Idara Usimamizi wa Deni la Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine, Kamishina wa Sera, Wizara ya Fedha, Dkt. Johnson Nyella, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Nuru Ndile na viongozi wengine waandamizi wa Serikali na Benki ya Dunia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news