Endeleeni kuiunga mkono Zanzibar katika utekelezaji wa miradi ya kipaumbele-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameishauri Benki ya Dunia kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kutekeleza miradi ya kipaumbele ya usambazaji wa maji, nishati ya umeme na ujenzi wa bandari.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo Juni 17,2025 alipokutana na ujumbe wa wataalamu kutoka Benki ya Dunia ulioongozwa na Mkurugenzi Mkaazi wa Benki hiyo nchini Tanzania, Nathan Belete ambao umefika Ikulu,Zanzibar.
Amesema kuwa sekta hizo tatu ni muhimu kwa maendeleo na ukuaji wa uchumi wa Zanzibar, hivyo Serikali imezichagua kuwa za kipaumbele kwa sasa, na kuishauri Benki ya Dunia kuisaidia Zanzibar kufikia malengo yake.

Akizungumzia nishati ya umeme, Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa Zanzibar inahitaji kuwa na umeme wake wa kujitegemea ili kukidhi mahitaji ya nishati hiyo sambamba na kupunguza gharama za ununuzi wa umeme.
Aidha, amebainisha kuwa Zanzibar inahitaji megawati 50 zaidi ili kuongeza nguvu kwenye megawati 120 zinazotumika hivi sasa, hatua itakayochochea ufanisi na kumaliza tatizo la mgao wa nishati hiyo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Nathan Belete, amepongeza kasi ya maendeleo ya miradi inayofadhiliwa na Benki hiyo Zanzibar na ushirikiano mzuri uliopo kati ya pande hizo mbili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news