Gharama ya kujaza gesi kwenye mitungi (LPG) ni himilivu-Mheshimiwa Kapinga

SIMIYU-Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema gharama ya kujaza gesi kwenye mitungi (LPG) ni himilivu ikiwa ni jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ili kuwezesha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.Mhe. Kapinga ameyasema hayo Juni 16, 2025 katika ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Simiyu wakati wa kuzindua Shule Maalum ya Sayansi ya Wasichana ya Simiyu ambayo imefungwa miundombinu ya nishati safi ya kupikia.

“Mheshimiwa Rais ulituelekeza taasisi ambazo zinahudumia watu zaidi ya mia moja tuzifungie miundombinu ya nishati safi ya kupikia, Wizara ya Nishati kwa kushirikiana na TAMISEMI tunatekeleza agizo hilo kwa kuzifungia mifumo ya nishati safi shule mpya ambazo zinajengwa,"amesema Kapinga.
Ameeleza kuwa, uwezo wa shule hiyo ni wanafunzi 800 na mifumo ya Nishati Safi ya Kupikia iliyofungwa ina uwezo wa kuhudumia wanafunzi 800.

Ameongeza kuwa, kwa idadi hiyo ya wanafunzi 800 mtungi wa gesi katika Shule ya Wasichana Simiyu utakuwa ukijazwa kila baada ya miezi miwili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news