DAR-Klabu ya Yanga Sc imethibitisha kuwa mnamo Juni 7, 2025 ilipokea barua kutoka Bodi ya Ligi Kuu Tanzania kwa ajili ya kuhudhuria kikao maalum cha kujadili masuala yahusuyo mchezo namba 184 wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga dhidi ya Simba na kubainisha kuwa uongozi wa klabu hiyo umetii wito huo.

“Baada ya majadiliano ya saa kadhaa, Viongozi wa Klabu waliwasilisha msimamo wa Klabu YETU kuwa hatutashiriki mchezo namba 184 uliopangwa kufanyika tarehe 15 Juni 2025 mpaka pale matakwa yetu tuliyoyawasilisha kwa maandishi kwao yatakapotimizwa.
“Tunawatakia kila la heri Bodi ya Ligi na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini katika kushughulikia matakwa yetu yenye mustakabali mkubwa kwenye maendeleo ya mpira wa miguu Tanzania;