Ukatili wa kingono,kihisia na kimwili kwa watoto wapungua Tanzania

NA GODFREY NNKO

UTAFITI mpya Tanzania umeonesha kuwa, matukio ya ukatili dhidi ya watoto na vijana nchini yamepungua huku sababu kuu zikitajwa kuwa zinachagizwa na jitihada za Serikali kwa kushirikiana na wananchi wakiwemo wadau katika kukomesha matukio ya kikatili.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ameyasema hayo leo Juni 9,2025 jijini Dar es Salaam wakati akitangaza matokeo ya Utafiti wa Kitaifa wa Ukatili dhidi ya Watoto na Vijana Tanzania (VACS-2024).

Amesema,utafiti huu ulilenga kupima kiwango cha ukatili wa kingono, kimwili na kihisia dhidi ya watoto na vijana wa kike na wa kiume nchini Tanzania na kuelewa hatari na athari za kiafya zinazohusiana na ukatili huu.

"Utafiti huu ulifanyika kati ya mwezi Machi na Juni, 2024 na uliwafikia zaidi ya watoto 11,414 wenye umri wa miaka 13 hadi 24 kutoka mikoa yote 31 ya Tanzania Bara na Zanzibar."

Amesema,kwa mujibu wa utafiti huo ambao umefanywa na watafiti wabobezi unaonesha kuwa, matukio ya ukatili wa kingono kwa watoto wa kike yamepunua kutoka asilimia 33 hadi 11.

Pia,matukio ya ukatili dhidi ya watoto wa kike yamepungua kutoka asilimia 76 hadi 24 huku ukatili wa kihisia matukio ya kikatili yamepungua kutoka asilimia 25 hadi 22.

Kwa upande wa watoto wa kike,Mheshimiwa Waziri Dkt.Gwajima amesema kuwa, matukio ya ukatili upande wa kingono yamepungua kutoka asilimia 21 hadi tano,kimwili kutoka asilimia 74 hadi 21.

Waziri Dkt.Gwajima ameongeza kuwa, kwa upande wa ukatili wa kihisia kwa watoto wa kiume matukio yamepungua kutoka asilimia 31 hadi 16.

Utafiti huo ni wa pili kufanyika ndani ya miaka 15 tangu ule wa kwanza wa Kitaifa kufanyika mwaka 2009 nchini.

Amesema, licha ya mafanikio hayo bado kuna vijana na watoto wa makundi mbalimbali wanapitia katika changamoto kadhaa ambapo, ushirikiano wa pamoja unahitajika ili kuhakikisha watoto wote wanalindwa na kuwezeshwa ili waweze kufikia ndoto zao.

Waziri Dkt.Gwajima amesema kuwa,matokeo ya utafiti huu yatawezesha Serikali na wadau kuboresha na kuandaa mipango, programu na mikakati mbalimbali ya kutokomeza ukatili nchini itayoimarisha ulinzi na usalama wa watoto na vijana na maslahi mapana ya kizazi cha sasa na cha baadae. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news