ZANZIBAR-Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation(ZMBF), Mhe. Mama Mariam Mwinyi ameushukuru uongozi wa Multi Click Digital Solutions Ltd kwa utayari wao kushirikiana na ZMBF katika safari ya mageuzi ya kidijitali yenye tija kwa maendeleo.
Mama Mariam Mwinyi amesema hayo alipokutana na Uongozi wa Multi Click Digital Solutions Ltd katika Ofisi zake Migombani, Mkoa wa Mjini Magharibi leo Juni 5,2025.Katika mazungumzo yao yalihusu kutumia teknolojia katika kuboresha ufanisi wa utoaji wa huduma bora kwa jami ikiwemo uanzishaji wa mifumo ya kidijitali kwa ajili ya utawala bora, usimamizi wa taarifa, na utoaji wa huduma rafiki kwa jamii.




