■Asema utoaji wa tuzo unalenga kuendeleza na kuimarisha sekta ya michezo nchini
DAR-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya mapinduzi makubwa katika sekta ya michezo kama sehemu ya utekelezaji wa Ibara ya 243 ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020.

“Ongezeko hili ni kubwa zaidi katika historia ya Wizara hii.”
“…Serikali imeendelea na mkakati wake wa kuhakikisha inainua michezo hapa nchini, kila mmoja kwa nafasi yake uwe mchezaji, wakala, mdhamini endelezeni taaluma hiyo. Leo hii tuna kila sababu ya kumpongeza na kumshukuru rais wetu kwa kufungua hiyo milango na kuongeza bajeti na kuruhusu sekta binafsi kushiriki kwenye michezo.”
Ameyasema hayo usiku wa Juni Mosi, 2025 katika hafla ya usiku wa tuzo zilizoandaliwa na Baraza la Michezo Tanzania kwa wanamichezo waliofanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa iliyofanyika katika Ukumbi wa The Super Dome, Masaki, jijini Dar es Salaam.