Mheshimiwa Kapera aapishwa katika Kikao cha 49 cha AUABC

ARUSHA-Kikao cha Kawaida cha 49 cha Bodi ya Umoja wa Afrika ya Ushauri Dhidi ya Rushwa (AUABC) kinafanyika jijini Arusha yalipo Makao Makuu ya Bodi hiyo kuanzia Juni 16, 2025 hadi Juni 21, 2025.
Mheshimiwa Benjamin akila kiapo Juni 16, 2025.

Katika siku ya kwanza ya kikao hicho, wajumbe wapya wa Bodi akiwemo Mhe Benjamin Kapera kutoka Tanzania waliapishwa. Wengine walioapishwa ni Mhe. Dkt Graciano Dominongos (Angola) na Mhe. Absatou Ly Diallo kutoka Senegal.

Mheshimiwa Benjamin Kapera kutoka Tanzania ambaye pia ni mtumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) alichaguliwa kuwa mjumbe Februari 13, 2025 katika mkutano uliofanyika Addis Ababa Ethiopia.
Kikao cha 49 kimeenda sambamba na uchaguzi wa na uongozi mpya wa Bodi ambapo Mwenyekiti aliyechaguliwa ni Mhe. Kwami Senanu kutoka Ghana, Makamu Mwenyekiti ni Mhe. Yvonne Chibiya kutoka Zambia na Katibu ni Mhe. Principe Ntibasume kutoka Burundi. Muda wa uongozi wa Bodi ni miaka 2 ambapo wajumbe wapya wanatarajiwa kutumikia kwa miaka 6.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news