Wajumbe wa Baraza la Kata ya Msitu wa Tembo Simanjiro mahakamani kwa rushwa

MANYARA-Katika Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro, Juni 13, 2025 limefunguliwa shauri la Jinani namba 14400/2025 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro,Mheshimiwa Onesmo Nicodemo.
Kesi hii ni ya Jamhuri dhidi Wajumbe wanne wa Baraza la Kata ya Msitu wa Tembo ambao ni Bw. Eliasi John Kimweri, Bw. Felister Ibrahimu Mphuru, Bw. Ally Petro Mphuru na Bw. Joseph Samson Simbeye.

Washtakiwa wanashtakiwa kwa kosa la kuomba na kupokea hongo kinyume na kifungu cha 15(1) (a) na 15(2) vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa sura ya 329 R.E 2022.

Akisoma hati ya mashtaka Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU,Bw. Faustin Mushi ameeleza kuwa,washtakiwa kwa kushirikiana, mnamo mwezi Mei 2025 walishawishi kwa kuomba na kupokea hongo ya kiasi cha shilingi 120,000 kutoka kwa Bw. Issa Ally Njuju ili waweze kumsaidia kushinda shauri la ardhi lililokuwa limefunguliwa katika Baraza hilo dhidi yake.

Washtakiwa wamekana kutenda makosa yote yanayowakabili na shauri limeahirishwa hadi Juni 25,2025 kwa ajili ya kusikilizwa Hoja ya Awali (PH).

Kwa sasa washtakiwa wote wanne wapo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news