BERLIN-Mwanamuziki Ebrahim Makunja anatarajia kutunukiwa tuzo ya Balozi wa Utamaduni Afrika (Ambassador of African Culture).
Tuzo hiyo inayotolewa na Africa We Want Organisation ya Ujerumani inatokana na kutambua mchango wa mwanamuziki huyo mtanzania kiongozi na mwanzilishi wa bendi maarufu ya The Ngoma Africa Band.
Bendi hiyo ina majina mengi yaliobatizwa na washabiki wake kama Viumbe imara wa ajabu "Anunnaki Alien's " kutoka special planet Bongoland, FFU Ughaibuni wakifananishwa na kikosi maalumu.Kikosi kazi hicho The Ngoma Africa Band chenye masikani kule Ujerumani ambayo kimeutangaza vema muziki wa kiafrika katika kila kona za kimataifa.