Mwanakijiji wilayani Tanganyika hatiani kwa kupokea hongo

KATAVI-Juni 17, 2025 Mahakama ya Wilaya ya Tanganyika imetoa hukumu dhidi ya Bw.Peter Gaga Ndilana mkazi wa kijiji na Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi.
Amehukumiwa adhabu ya kulipa faini ya shilingi 500,000 au kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kupokea hongo ya shilingi 800,000 kinyume na Kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa sura ya 329 Marejeo ya 2022.

Hukumu hii imetolewa katika Kesi ya Jinai namba 14290/2025 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mh. Sydney William Nindi.

Kesi hiyo imeendeshwa na Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU),Amos Mwalwanda.

Awali akisoma mashtaka mahakamani hapo Bw. Amos Mwalwanda alisema,mshtakiwa alipokea fedha kiasi cha sh. 800,000 kutoka kwa John Marco Nyanda ili asimfikishe Kituo cha Polisi ambako awali alikuwa amepewa RB ili akamatwe aweze kujibu mashtaka yanayomkabili.

Baada ya kufikishwa mahakamani na kusomewa makosa yanayomkabili mshtakiwa alikiri kutenda kosa hilo ndipo alipohukumiwa kulipa faini ya sh. 500,000 au kwenda jela miaka mitatu.Mshtakiwa amelipa faini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news