UN yaitaja Tanzania mfano wa kuigwa mapambano dhidi ya rushwa Afrika

VIENNA-Serikali ya Tanzania imepongezwa na Umoja wa Mataifa (UN) kwa jitihada za kuzuia rushwa. Pongezi hizo zimetoleaa wakati wa Kikao cha 16 cha Wataalam cha kutathmini utekelezaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kuzuia Rushwa kilichoanza Juni 16 hadi 20,2025 jijini Vienna.
Aidha,pongezi hizo zilitolewa baada ya Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Ununuzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Bw. Charles Birore kuwasilisha taarifa ya nchi namna Mfumo wa Kieletroniki wa Ununuzi wa Umma (NeST) ulivyosaidia kupunguza mianya ya rushwa katika ununuzi wa umma.

Katika hatua nyingine, Tanzania imepongezwa kwa kuondolewa kwenye Orodha ya nchi zenye mapungufu ya kimkakati katika mifumo ya udhibiti utakatishaji fedha haramu, ufadhili wa ugaidi na ufadhili wa silaha za maangamizi (Grey List).
Akitoa taarifa ya nchi ya utekelezaji wa Mkataba wa UNCA, Mkurugenzi wa Uchunguzi na Kiongozi wa Timu ya Wataalamu kutoka Tanzania, Bw. Simon Maembe alieleza kuwa, maboresho makubwa ya mifumo ya udhibiti wa fedha haramu yamepelekea Kikosi Kazi cha Kifedha cha Kimataifa (FATF) mwishoni mwa Mkutano Mkuu wa FATF uliofanyika katika Mji wa Strasbourg nchini Ufaransa tarehe 10 hadi 13 Juni 2025 kutangaza kuiondoa Tanzania kwenye orodha hiyo.

Kutoka TAKUKURU kikao hiki kinahudhuriwa na Mkurugenzi wa Uchunguzi, Bw. Simon Maembe pamoja na Gabriella Gabriel kutoka Kurugenzi ya Elimu kwa Umma.
Wengine kutoka Tanzania ni Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Austria, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma, Wizara ya Katiba na Sheria, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka-Divisheni ya Makosa ya Udanganyifu, Utakatishaji Fedha na Rushwa pamoja na Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news