Mwanasheria Mkuu wa Serikali awasilisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2025
DODOMA-Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza S. Johari leo Juni 5,2025 bungeni jijini Dodoma amewasilisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2025 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2025).
Mwanasheria Mkuu wa Serikali amewasilisha Muswada huo katika Mkutano wa Kumi na Tisa,Kikao cha Arobaini cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloendelea bungeni jijini Dodoma.