IRINGA-Timu ya soka ya Wasichana maalumu kutoka Mkoa wa Mwanza, imeibuka na ushindi mnono dhidi ya Pwani katika Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Tanzania kwa Shule za Msingi na Sekondari yanayoendelea mkoani Iringa.

Mwanza imeshinda kwa Jumla ya magoli 5-0 hivyo kuifanya kujiweka vizuri kusonga mbele katika hatua zinazofuata.
Kwa upande wa Soka maalumu Wavulana, timu ya soka ya Mkoa wa Dar es salaam, ilipata ushindi mnono baada ya kuifunga Shinyanga jumla ya magoli 5-1.
Michezo hiyo ya soka maalumu wasichana na wavulana, iko kwenye hatua ya Makundi na inatarajiwa kuendelea Juni 12,2025 katika viwanja vya Kichangani.
Mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA 2025, yanaratibiwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI, ikishirikiana na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, pamoja na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.