MWANZA-Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mkoa wa Mwanza, tarehe 10 Juni 2025 imekutana na kufanya kikao na wakuu wa vitengo vya sheria wa halmashauri za Mkoa wa Mwanza.
Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mjini Mwanza na kimeongozwa na Wakili wa Serikali wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Kadyemela Lushagara

Lengo la kikao hicho ilikuwa ni kukutana na Wakuu wa Vitengo vya Sheria Mkoa wa Mwanza na kuwafahamisha juu ya uwepo wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Mkoa wa Mwanza na huduma za kisheria zitolewazo na Ofisi hiyo.

Ushiriki wao katika zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, 2025.