DODOMA-Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ni miongoni mwa taasisi za umma ambazo zimeshiriki katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma Juni 17,2025 ambayo yanaendelea katika viwanja vya Chinangali kuanzia Juni 16 hadi 23,2025.
Watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, wakiwa na Bango la kauli mbiu kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma tayari kwa kushiriki ufunguzi wa Maadhimisho hayo yanayoendelea jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akifungua Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa umma wakati wa Ufunguzi wa Maadhimisho hayo uliofanyika jijini Dodoma.

Watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayuko pichani) wakati akifungua Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa umma yanayoendelea jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Juma Mkomi akitoa salamu za Ofisi hiyo wakati wa Ufunguzi wa Maadhimisho hayo uliofanyika jijini Dodoma.
Tags
Habari
Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali
Picha
Picha Chaguo la Mhariri
Wiki ya Utumishi wa Umma Tanzania