Rais Dkt.Samia atembelea mradi wa REA mkoani Simiyu

SIMIYU-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametembelea mradi wa nishati safi ya kupikia wa shule ya Sekondari ya Wasichana Simiyu iliyopo Bariadi mkoani humo na kupewa maelezo na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga wakati akifungua shule hiyo leo tarehe 16 Juni, 2025.
Mradi huo unahusisha usimikaji wa mfumo wa kupikia kwa kutumia gesi yaani LPG, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa, hivyo kuchangia katika utunzaji wa mazingira na kulinda afya ya wanafunzi na walimu.

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imetoa ufadhili wa kiasi cha Shilingi Shilingi Milioni 14 kwa ajili ya ujenzi na usimikaji wa miundombinu ya nishati safi ya kupikia katika shule hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news