ARUSHA-Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ametembelea na kukagua maendeleo ya miradi wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu unaojengwa katika kata ya Olmoti jijini Arusha utakaotumika katika mashindano ya AFCON 2027.
Karia ametembelea uwanja huo akiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Methusela Ntonda na viongozi wengine wa Wizara hiyo Mei 30, 2025 na kuweza kuona maendeleo ya ujenzi.