Kesi ya Tundu Lissu kurushwa mubashara

DODOMA-Mahakama ya Tanzania imesema Shauri la Jinai Namba 8606/2025 na Namba 8607/2025 kati ya Jamhuri na Tundu Lissu, ambayo yamepangwa kutajwa na kusikilizwa Juni 2, 2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mwenendo wote utarushwa mubashara (live) na pia Mshtakiwa atafikishwa Mahakamani.
Taarifa ya Mahakama imeeleza, lengo ni kuwawezesha Wananchi kufuatilia bila kuwa na ulazima wa kufika Mahakamani, pia ni Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania kuimarisha uwazi, uwajibikaji na matumizi ya teknolojia katika huduma ya utoaji haki.

Taarifa imeeleza Mahakama ya Wazi Kisutu ni ndogo, inachukua Watu 80, hivyo imekubalika watakaoingia ni Mawakili wa Serikali na Watu wengine (10), Mawakili Utetezi na Watu wengine (60) na Waandishi wa Habari (10).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news