DODOMA-Serikali imesema kuwa, inaendelea kufuatilia kwa makini sakata la mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Yanga na Simba, lakini haitangilia moja kwa moja kuepuka vikwazo vya FIFA huku ikisisitiza kanuni na sheria zilizowekwa za uendeshaji wa mpira zifuatwe.

"Tunafuatilia kwa ukaribu namna mgogoro unavyoendelea kutatulia huku tukijaribu kwa kiwango kikubwa kutoingilia maamuzi ya TFF na bodi ya ligi na tunasisitiza mamalaka kufuata kanuni na sheria walizojiwekea za Mpira wa miguu,” amesema Mhe. Hamis Mwinjuma