DAR-Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema kuwa, baada ya mafanikio makubwa ya uendeshaji wa treni za SGR ambapo mpaka kufikia Juni 2025, zaidi ya abiria milioni 2.5 wamesafirishwa kwa treni hiyo toka kuanza uendeshaji wake Juni 14, 2024 sasa linaanza kusafirishaji mizigo.
Shirika limeeleza kuwa kuanzia Juni 27, 2025 litaanza rasmi huduma ya usafirishaji wa mizigo kwa njia ya Reli ya kisasa ya SGR kati ya Stesheni ya Pugu Dar Es Salaaam na Stesheni ya Ihumwa, Dodoma, ambapo kwa kuanza kutakuwa na treni moja kila siku.

