DODOMA-Treni ya kwanza ya mizigo ya reli ya kiwango cha kimataifa ( SGR) ikiwasili Ihumwa, Dodoma majira ya mchana, ikitokea stesheni ya Pugu, Dar es Salaam.
Treni hiyo yenye mabehewa 10 iliyobeba tani takribani 700 za mizigo mbalimbali imetimiza ahadi ya kuanza huduma ya usafiri wa treni za mizigo katika reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) na Tanzania kuweka historia kwenye ukanda wa Afrika Mashariki kuwa na treni ya mizigo ya SGR .



