Tumieni sauti na kalamu zenu kuelimisha wananchi kuhusu masuala ya mnyororo wa ugavi-Dkt.Mwakibinga

NA GODFREY NNKO

KAMISHNA wa Idara ya Sera za Ununuzi wa Wizara ya Fedha,Dkt.Frederick Mwakibinga amewahimiza waandishi wa habari nchini kuendelea kutumia sauti na kalamu zao kuelimisha umma kuhusu masuala ya mnyororo wa ugavi.
“Nimefarijika pia, kwa kuona mwitikio mkubwa wa nyie kushiriki katika mafunzo haya,mwitikio huu unaonyesha dhamira ya pamoja ya kuendeleza ushirikiano kati ya Wizara ya Fedha na nyie wanahabari.

"Kama mnavyofahamu nyie ndio sauti na sauti unaweza kuitumia vyovyote unavyotaka unaweza kutumia kujenga au kubomoa," amesisitiza  Dkt.Mwakibinga huku akiwataka wanahabari kuzitumia sauti na kalamu zao kujenga.
Dkt.Mwakibinga ameyasema hayo leo Juni 18,2025 mkoani Morogoro wakati akifungua semina kwa wamiliki na waandishi wa habari za mitandaoni wanaoandika habari za Wizara ya Fedha ambapo wamejengewa uelewa kuhusu masuala ya mnyororo wa ugavi.

Amesema, Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kamilifu kupitia mnyororo wa ugavi.

Dkt.Mwakibinga ametolea mfano kuwa, zaidi ya asilimia 70 ya bajeti ya Serikali hutumika katika kununua vifaa na huduma kwa ajili ya kuwahudumia wananchi kote nchini.
Vilevile amebainisha kuwa, fedha hizo ambazo zinafanya shughuli hiyo zinapatikana kupitia mnyororo wa ugavi toka fedha zinatoka, mahitaji ya ununuzi yanatengenezwa vinavyonunuliwa, kupokelewa, kusambazwa hadi kumfikia mtu wa mwisho.

“Hizo hatua zote ndizo zinatengeneza mnyororo wa ugavi,na hivyo vitu vinatakiwa viwe na muunganiko ambao utatengeneza flow ambayo itakuwa na manufaa.”
Dkt.Mwakibinga amesema,muunganiko huo hautakuwa umekaa vema iwapo patakuwepo kasoro huko njiani,kwani mwisho wa siku ukamilifu wa kilichokusudiwa hautafikiwa.

“Kupitia kwenu ningependa kuwafikia wananchi wa Tanzania waweze kuufahamu vizuri umuhimu wa huo mnyororo na hivyo kuweza kujipanga na kuusimamia vizuri ili uwe na matokeo yanayotarajiwa."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news