NA AHMED ALLY
Msemaji Simba SC
MWAKA 2011 PSG ilininunuliwa na Qatar Sports Investments kwa hisa za asilimia 87.5 baada ya hapo Tajiri amejaribu kutawala soka la Ulaya lakini hakufanikiwa
Safari yake imeenda sambamba na kusajili wachezaji wakubwa duniani kama Messi, Neymar na wengineo lakini bado hakufikia malengo
Miaka 14 baada ya uwekezaji wake ndio PSG imefanikiwa kubeba Ubingwa Ulaya.
Pyramdis ilinunuliwa na Tajiri kutoka Falme za kiarabu (UAE) Salem Al Shamsi mwaka 2019.
Baada ya Al Shamsi kuinunua Pyramids imemlazimu kusubiri kwa miaka sita kuchukua ubingwa wa Afrika
Njia ya Tajiri wa PSG na Pyramids ndio anayopitia tajiri wa Simba Sports,Mohamed Dewji (Mo Dewji).
Mo Dewji ameingia rasmi Simba mwaka 2018 akiwa Mwekezaji wa hisa 49, ndani ya miaka saba ya uwekezaji wake Simba imecheza Fainali ya Afrika.
Hii ni hatua kubwa sana kwa Simba na Mo Dewji kwenye malengo yao kutawala soka la Afrika.
Muhimu kwetu wana Simba ni kuwa na subira, ukubwa wa Afrika ndio kitu tunachokitafuta hivi sasa na hatupo mbali kufikia
Tumpe support mwekezaji wetu kama walivyofanya PSG na Pyramids na tuendelee kuinga mkono timu yetu bila kuchoka.