Ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Nkangamo-Momba kukamilika Mei mwaka ujao

DODOMA-Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema, ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Nkangamo- Momba unatarajiwa kukamilika Mei mwakani.
Mheshimiwa Kapinga ameeleza hayo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Momba, Condester Sichalwe (CCM) ambaye aliuliza ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Kituo cha kusambaza umeme Nkangamo-Momba.

Amesema, ujenzi wa kituo hicho cha Nkangamo-Momba ulianza mwezi Mei, 2024 ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 30.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news