Waziri Balozi Kombo ampokea Rais Ndayishimiye

DODOMA-Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo amempokea Rais wa Jamhuri ya Burundi Mheshimiwa Evariste Ndayishimiye aliyewasili nchini kwa ajili ya kushiriki uzinduzi wa Kiwanda cha mbolea cha Itra-Com kilichopo eneo la Nala jijini Dodoma.

Mheshimiwa Ndayishimiye ambaye ameambatana na mwenza wake Mhe. Mama Angeline Ndayishimiye pamoja na Viongozi waandamizi kutoka Serikali ya Burundi aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa jijini Dodoma na kulakiwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na baadaye kuelekea Nala ambako yeye na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan watashiriki uzinduzi wa Kiwanda hicho ambacho mwekezaji ni raia kutoka Burundi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news