MOROGORO-Chuo Kikuu Mzumbe kinapenda kuwataarifu Wanafunzi, wazazi na Wadau wa elimu kitakuwa na Kambi Maalumu za Udahili kwa mwaka wa masomo 2025/2026 kuanzia tarehe 13 hadi 22 Julai 2025, katika mikoa ifuatayo;
Dar es Salaam - Mlimani City Mall
Mwanza – Rock City Mall
Dodoma – Viwanja vya Nyerere Square
Arusha – Uwanja wa Makumbusho
Mbeya - Stendi ya Kabwe
Huduma zitakazotolewa ni Pamoja na; Elimu ya uchaguzi wa kozi na vigezo vya kujiunga, Ushauri wa kitaaluma kwa wanafunzi watarajiwa (Career guidance),huduma ya udahili wa papo kwa hapo.
Hii ni nafasi ya kipekee kwa wazazi, wanafunzi na wadau wa elimu kufika na kupata huduma za moja kwa moja katika msimu huu wa dirisha la udahili kwa Wanafunzi wa elimu ya juu kutoka kwa Maafisa mahiri wa Chuo Kikuu Mzumbe.
Huduma zitatolewa kila siku kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni.Hakuna kiingilio na ushauri unatolewa bila malipo.
Wadau wote mnakaribishwa.Kwa taarifa zaidi, tafadhali tufuatilie katika mitandao yetu ya kijamii na tovuti ya Chuo Kikuu Cha Mzumbe.
Karibu Chuo Kikuu Mzumbe, “Tujifunze kwa Maendeleo ya Watu”
