Gavana Tutuba aikaribisha Absa Group kuendelea kuwekeza katika sekta ya fedha nchini

DAR-Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba ameikaribisha Absa Group kupitia kampuni zake kuendelea kuwekeza katika sekta ya fedha nchini.
Ameyasema hayo leo Jumanne Julai 22, 2025 alipokutana na kufanya mazungumzo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Absa Group, Bw. Kenny Fihla katika ofisi ndogo za Makao Makuu ya Benki Kuu jijini Dar es Salaam.

Akimkaribisha kuwekeza katika sekta ya fedha, Gavana Tutuba amesema; "Tanzania kuna mazingira rafiki ya kufanyia biashara na kuendelea kuimarika kwa uchumi wa Tanzania.
"Ripoti kutoka Kampuni ya Kimataifa Inayojihusisha na Kufanya Tathmini ya nchi kukopesheka katika masoko ya mitaji ya kimataifa ya Fitch Ratings inaonesha Tanzania ipo katika daraja la B+ ikionesha mwenendo mzuri wa uchumi,"ameongeza Gavana Tutuba.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Absa Group, Bw. Fihla ambaye ameteuliwa hivi karibuni ameipongeza Benki Kuu kwa usimamizi thabiti wa sekta ya fedha na uchumi wa nchi kiujumla.

Absa Group kwa Tanzania pia inamiliki hisa nyingi katika Benki ya NBC.
Mkutano huo pia umehudhuriwa pia na Naibu Gavana (Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha),Bi. Sauda Msemo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Bw. Theobald Sabi na Mkurugenzi Mtendaji wa Absa Group kwa ukanda wa Afrika, Saviour Chibiya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news