Gavana Tutuba aongoza wafanyakazi wa BoT kushiriki NBC Dodoma Marathon

DODOMA-Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba ameongoza wafanyakazi wa BoT kushiriki katika mbio za NBC Dodoma Marathon 2025 zilizofanyika leo, tarehe 27 Julai 2025, jijini Dodoma.
Katika mbio hizo zilizowakutanisha washiriki kutoka sekta mbalimbali, wafanyakazi wa BoT walishiriki katika makundi tofauti ya mbio, ikiwemo kilomita 5, 10, 21 na 42.
Ushiriki wa Benki Kuu katika mbio hizo unaonesha dhamira ya BoT si tu katika masuala ya uchumi na fedha, bali pia katika kuwekeza kwenye afya ya rasilimali watu wake na kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za kijamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news