Utenzi wa pongezi kwa wahitimu wa kidato cha Sita wa mwaka 2025 ambao matokeo ya mitihani yao yametangazwa tarehe 06 Julai, 2025 na Baraza la Mitihani la Tanzania.
¹Pongezi kwenu cha Sita
Matokeo kuyapata
Masomo 'liyafumbata
Mmefaulu kishindo
²Hakika mlijikita
Masomo kuyachakata
Leo hii metakata
Ufaulu wa kishindo
³Masomo mlikamata
Juhudi mkazingata
Hakika mmekung'uta
Ufaulu maridhawa
⁴Pokeni zetu pongezi
Kwa nzurisa' yenu kazi
Hamkufanya ajizi
Mmetisha kwa kishindo
⁵Pongezi pia wazazi
Jamii wote walezi
Ni wao wema ulezi
Mmeshinda kwa kishindo
⁶Heko kwao viongozi
Kwa shule usimamizi
Na walimu chapakazi
Cha Sita mmetusua
⁷Sasa muipande ngazi
Ya maarifa ujuzi
Pamoja na ubobezi
Chuo Kikuu Huria
⁸Huria cha Tanzania
Pongezi chawapatia
Na heko twairudia
Kongoleni wahitimu
MTUNZI
Dkt. Mohamed Maguo
Mhadhiri Mwandamizi
Mkuu wa Itifaki
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
.jpeg)