IJP Wambura atembelea banda la Mwanasheria Mkuu wa Serikali maonesho ya Sabasaba

DAR-Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IJP),Camilius Wambura tarehe 6 Julai, 2025 ametembelea Banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inashiriki maonesho hayo kwa kutoa huduma ya Elimu ya Sheria, Ushauri wa Kisheria, Kughulikia Malalamiko na Utatuzi wa Migogoro, ambapo Banda la Ofisi liko katika Mtaa wa Media, Hema la Jakaya Kikwete banda namba 24.
Maonesho ya Sabasaba yenye kauli mbinu ya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba Fahari ya Tanzania yalianza tarehe 28 Juni , 2025 na yanatarajiwa kumalizika tarehe 13 Julai, 2025.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news