Kuna ongezeko kubwa la makusanyo ya kodi nchini-Waziri Dkt.Nchemba

ARUSHA-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa, kuna ongezeko kubwa la makusanyo ya kodi mara tu baada ya Serikali ya Awamu ya Sita kuingia madarakani ambapo kwa mwaka wa fedha 2021/22, TRA ilikusanya shilingi trilioni 22.2.
Pia, mwaka wa fedha 2022/23 ilikusanya shilingi trilioni 24.1,mwaka wa fedha 2023/24, ilikusanya shilingi trilioni 27.6 na kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 2024/25 imeshuhudiwa kiasi cha shilingi trilioni 32.26 sawa na ufanisi wa asilimia 103.9 kutoka lengo la kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 31.05.

Mhe. Dkt. Nchemba, ameyasema hayo wakati akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, kufungua rasmi Kikao Kazi cha Tathimini ya Utendaji kazi cha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), katika Mwaka wa Fedha 2024/2025, kinachofanyika kwa siku tano katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), jijini Arusha.
Alibainisha kuwa, makusanyo hayo yamewezesha kufadhili miradi mbalimbali ya kimkakati ya maendeleo na akatumia fursa hiyo kuipongeza Menejimenti na watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kujituma na kufanya kazi kwa weledi, uaminifu na uwajibikaji mkubwa waliouonesha katika kufanikisha malengo hayo.
Aliwataka watumie kikao kazi hicho kuweka mikakati thabiti ya utendaji kazi ili kuongeza ufanisi na tija katika kufikia malengo zaidi ili kuendelea kuchangia maendeleo kwa masilahi mapana ya ujenzi wa Taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news