Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetoa ufafanuzi kuhusu tukio la kijana kudaiwa kuchomwa visu na vijana wa mtaa mmoja katika eneo la Jeshini, Mbagala, lililosambaa kwenye mitandao ya kijamii kupitia video ya baba wa kijana huyo.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Polisi, tukio hilo lilitokea tarehe 22 Juni 2025 majira ya saa 2 usiku ambapo Osama Khamis Mohamed (18), mkazi wa Mwembemtongo, Tuangoma, Temeke alijeruhiwa kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kisu baada ya kutokea ugomvi kati yake na vijana wenzake wanne kutoka mtaa mmoja. Chanzo cha ugomvi huo kilitajwa kuwa ni deni la shilingi 2,000/= ambapo majeruhi alidaiwa kiasi hicho, na aliposhindwa kulipa, simu yake ya mkononi ilinyang’anywa kwa nguvu.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo



































