Magazeti leo Julai 11,2025

Wadau wa sekta binafsi mkoani Tabora wamewasilisha maoni na mapendekezo yao kwa Timu ya Kitaifa ya Wataalamu inayoratibu maandalizi ya awamu ya pili ya Mpango wa Maboresho ya Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (MKUMBI II), ambayo ipo mkoani humo kwa ajili ya kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali.
Timu hiyo inaendelea na kazi ya ukusanyaji wa maoni kutoka kwa wadau kwa lengo la kutambua mafanikio yaliyopatikana pamoja na changamoto zinazokwamisha biashara na uwekezaji nchini.

Lengo la zoezi hili ni kuhakikisha kuwa mchango wa sekta binafsi unazingatiwa kikamilifu katika kubaini maeneo ya kipaumbele na kuweka mikakati madhubuti ya maboresho ya sera pamoja na mazingira ya biashara na uwekezaji kwa ujumla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news