Singida Black Stars imethibitisha kumsajili mshambuliaji Andrew Simchimba, ambaye alikuwa Mfungaji Bora wa Ligi ya Championship 2024/2025, akitokea Geita Gold FC.
Simchimba alifunga mabao 18 katika mechi 20 za Championship 2024/2025, sawa na Raizin Hafidh wa Mtibwa Sugar na Abdulaziz Shahame wa TMA Stars, ambao pia walifunga mabao 18.“Tumemuongeza kikosini mshambuliaji hatari, Andrew Simchimba, ambaye ni Mfungaji Bora wa Ligi ya Championship 2024/2025,” imeeleza taarifa ya Singida BS.










Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo












