WARATIBU wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) katika mikoa ya Lindi na Mtwara wametakiwa kutojihusisha na makundi mbalimbali ya Whatsapp kipindi hiki wanapoelekea katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba,2025.
Hayo yamejiri Julai 17 wakati wa kufunga mafunzo ya siku tatu kwa waratibu hao yaliyofanyika kwenye Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara.
Akizungumza kwa niaba ya Mjumbe wa INEC, Mratibu wa Mafunzo wa INEC, Cecilia Sapanjo amesema katika kipindi hicho cha mchakato huo wa uchaguzi wasijihusishe kutuma taarifa yoyote kwenye makundi hayo kwani kufanya hivyo ni kutenda kosa chini ya sheria na watawajibika kwa kosa hilo.
"Hivi sasa yapo magrupu mengi ya Whatsapp jitahidini katika kipindi hiki tuyapunguze ili tusije kukosea tukatuma taarifa yoyote katika magrupu haya,"amesisitiza Cecilia.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo























