Magazeti leo Julai 22,2025

JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia askari wake wawili kwa tuhuma za kumfyatulia risasi na kumsababisha kifo mwananchi aitwaye Frank Sanga, Julai 19, 2025, wakati wakiwa katika doria ya pikipiki katika eneo la Ntyuka, jijini Dodoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Agathon Hyrera, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo Julai 21, 2025, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini humo.
Kamanda Hyrera amesema,tukio hilo lilitokea majira ya saa 8:00 mchana katika Kata ya Ntyuka, ambapo askari hao walimkamata marehemu Frank Sanga akiwa anaendesha pikipiki bila leseni wala kuvaa kofia ya usalama, huku akiwa amebeba magunia matatu ya mkaa.

"Baada ya kukamatwa, askari walimuelekeza waende wote kituoni ili makosa yake yashughulikiwe kisheria. Hata hivyo, alikataa na kudai hawezi kwenda mpaka ndugu zake wafike," amesema Kamanda Hyrera.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news