Magazeti leo Julai 23,2025

Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imeshiriki zoezi la ukaguzi na majaribio ya mtambo utakaotumika kuchimba visima vitatu vya gesi asilia katika Kitalu cha Mnazi Bay mkoani Mtwara.
Ukaguzi huo uliofanyikia katika Jimbo la Tianjin nchini China, ulilenga kuhakiki uimara na ufanisi wa mtambo huo kabla ya kusafirishwa kuja nchini Tanzania kwa kazi ya uchimbaji wa visima vya gesi asilia inayotarajiwa kuanza Novemba 2025.
Pamoja na ukaguzi wa mtambo huo wenye uwezo wa kuchimba hadi urefu wa mita 8000, PURA pia ilishiriki kama muangalizi katika ukaguzi na majaribio ya mifumo mbalimbali iliyopo katika mtambo huo na mabomba yatakayotumika wakati wa uchimbaji.

Hatua hii ya ukaguzi ni muhimu kwa kuwa hutoa hakikisho la ufanisi wa mtambo kabla ya kuanza kwa utekelezaji wa mradi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news